Welcome to Pasiansi Alumni Association.

Welcome message.!

Dear Alumni, welcome to Pasiansi Alumni Association, this is the group of all members who finished their

Latest News

TAASISI YA TAALUMA YA WANYAMAPORI -PASIANSI CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI PASIANSI-MWANZA SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) KWA AJILI YA MIAKA 50 YA TAASISI Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi inayo furaha kuyatangazia makampuni yote yaliyosajiliwa pamoja na watu binafsi wenye uzoefu wa kutengeneza nembo (Logo) kuingia katika shindano la kutengeneza nembo (Logo) kwa ajili ya miaka 50 ya Taasisi. Uzinduzi wa maandalizi hayo utafanyika wakati wa mahafali ya miaka 50 ya Taasisi, tarehe 13 Juni, 2015, na maadhimisho rasmi yatafanyika mwezi Juni, 2016 sambamba na mahafali ya 51 ya Taasisi. DIRA YA TAASISI: Kuwa kitovu cha ufanisi katika kutoa mafunzo stahili ya Hima Sheria kwa ajili ya usimamizi endelevu wa wanyamapori. DHIMA YA TAASISI: Kuzalisha askari wanyamapori bora watakaoweza kulinda raslimali ya wanyamapori, kupitia mafunzo ya kijeshi, usimamizi wanyamapori, hima sheria na ulinzi pamoja na huduma za utafiti. Vigezo vifuatavyo vitatakiwa kuzingatiwa katika uandaaji wa nembo (Logo) hiyo: Majukumu ya Taasisi, kutimiza miaka hamsini (50) ya Taasisi, rangi ya Taasisi iwe ya kijani, njano (light yellow), Nembo (Logo) iwe inasomeka vizuri, kubuni kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi kwa kuzingatia dira na dhima ya Taasisi. Mshindi katika shindano hilo, atajishindia kiasi cha fedha taslimu (TZS) milioni mbili (2,000,000/=). Washiriki wote watatakiwa kuwasilisha nembo (Logo) watakazoandaa kabla ya tarehe 05/03/2015. Watumishi wa Taasisi hawaruhusiwi kushiriki katika shindano hili. Taasisi inawatakia ushiriki mzuri katika shindano hili. Read more


Latest News

Helloww,. Read moreBack to Top